CHAGUA
UZIMA
NA UISHI
Huduma ya Nan Ragland.
Chagua Uzima na uishi
Kimetolewa kwa upendo mkuu kwa Baba wa mbinguni.
Haki ya kunakiliwa
ISBN 1- 878957 – 00-07
Ili kupokea nakala ya ziada ya chagua nguve na uishi
Andika
Huduma ya Nan Ragland
Sanduku la Posta 77
Jackson, Mississippi 39205
Sadaka ya kugharamia utumaji, utunzaji na kurejesha (nakala nyingine) itapokelewa ingawa haihitajiki
Haki zote za kunakili yaliyomo zimenhifadhiwa chini ya sheria ya kimaifa ya haki za unakili.
Chagua uzima na uishi
Na
Joe na Nan Ragland.
Muumba wetu Mungu ndiye mpeanaji wa vipawa vyote vyema na vikamilifu, akiwa hana upendeleo
wa watu yeye in mwema kwa wote na Rehema zake ziko kwa kazi zake zote – ukiwemo wewe!.
Mungu si mwanzilishi wa maovu na kushindwa. Vivyo hivyo hana mambo hayo ili kupoeana. Maovu na maafa katika maisha hayatoki kw muumba wetu mpendwa, bali kwa adui wa mwanadamu Shetani na Roho zake as kipepo. Mungu alimtuma Yesu ili kuharibu kazi za adui wetu na kupeana uzima tele.
Mwivi (Shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi (Yesu) nalikuja ili wawe na uzima kasha wawe nao tele (Yohana 10:10).
Kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi (I Yohana 3:8)
Mungu amepean njia kwa ajili yako ili uwe huru kutoka kwa nguvu za shetani na dhamibi. Ameunda mpango mkuu ambao, unapofuatwa huhakikisha ushindi na uzima tele – sasa na nyakati zijazo. Tunaamini kuwa kwa kuusoma ujumbe huu, utaelewa toleo na mapenzi ya ajabu ya Mungu – chagua uzima.
Nimekuwekea mbele yako uzima na mauti--- basi chagua uzima, ili uwe hai.
(Kumbukumbu la torati 30:19.
Yeye aliye naye mwana anao huo uzima; asiye naye mwana wa Mungu hana huo uzima (I Yohana 5:12).
SURA 1
Utaishi milele.
Neno la Mungu la funza kuwa wewe ni kiumbe mwenye sehemu tatu:
(i) Roho na (2) Nafsi na (3) Miili yenu mhifadhiwe bila lawama- - - ( I Wathesalomike 5:23)
Ili kueleza zaidi:
Wewe ni roho
Una nafsi (nia, hisia, hiari)
Unaishi katika mwili
Wengi hupean muda na umaakini kwa miili na nia zao, pasipo kuzingatia thamani kuu ya Roho zao milele, ambapo hutoka chemichemi ya uzima.
Mtu wako wa Rohoni, mtu wa ndani, ndiye mtu wako wa kweli – ile sehemu hako ambayo haitawahi kukoma kuishi. Mwili wa kawaida ufapo, Roho yako itaendelea kuishi milele kwa sababu Roho haiwezi kufa.
Hata hivyo, swala ni ikiwa utachagua kuishi milele na Mungu, au utaondolewa uweponi mwake milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele… (Warumi 6:23).
Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. ( ufunuo 20:15)
(Wengi) watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. (Mathayo 25:46)
SURA 2
Haki hutokea tu kupitia kuzaliwa tena kwa Roho yako
Haki inamaanisha kuwa mtu ana msimamo wa sawa mbele ya Mungu. Mungu hukuona, na kukuitikia kama kwamba hukuwahi kutenda dhambi!
Pasipo kuzingatia matendo mema na tabia bora, wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. (I Yohana 1:8)
Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:25)
Unaweza tu kufanyika mwenye haki na upokee karama ya Mungu ya uzima wa milele kwa kumkubali Yesu kama mwokozi na Bwana wako. Imani katika Jina la Yesu Kristo ndio njia ya pekeeya kupata wokovu na msimamo wa sawa na Mungu.
Si kwa sababu ya matendo yetu ya haki tuliyotenda sisi; bali kwa rehema zake, alituokoa (Tito 3:5)
Hapana jina jingine (Ila Yesu Kristo) …. Walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo (Matendo 4:12)
SURA 3
Kuzaliwa upya hutokea to kupitia Yesu Kristo.
Mungu alimtuma mwanawe, Neno lililofanyika mwili, katika ulimwengu. Yesu aliyezaliwa na bikira alikuwa Mungu na mwanadamu.
Hapo mwanzo kulikwako Neno (Yesu) naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Yohana 1:1
Tazama bikira atachukua mimba …. naye atamwita jina lake Imanueli, yaani Mungu pamoja nasi. Isaya 7:14, Mathayo 1:23
Mungu alidhihirishwa katika mwili, …Akaaminiwa katika mataifa, Akachukuliwa juu katika utukufu
I Timotheo 3:16
Yesu aliishi maisha yasiyo lawama – jambo ambolo hakuna mwingine angefanya. Halafu kwa hiari yake akafanyika dhabihu, akiimwaga damu ya maish yake msalabani ili kulipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu. Akiisah kufa na Kuzikwa, Yeus alifufuliwa kihalisi kutoka kwa wafu siku ya tatu na Baba yake.
Yesu huyo, Mungu alimfufua, nasisitu mashahidi wake. (Matendo 2:32)
Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo … I Wakorintho 15:15
(Yesu) alidhihirishwa kwa mwana wa Mungu … kwa ufufuo (wake) wa wafu.
(Warumi 1:4)
Kufuatia ufufuo wake, Yesu alionekana na mashahidi zaidi ya mia tano katika kipindi cha siku arobaini, Baadaye akapaa mbinguni na sasa yuko katika mkono wa kulia wa Mungu Baba.
Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu … alizikwa na ya kuwa alifufuka siku ya tatu . . . Baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya miatano pamoja …I Wakorintho 15:3-6
(Yesu) Aliwadhihirisha nafsi yake ya kwamba yu hai (kutoka kwa wafu) kwa dalili nyingi akiwatokea muda wa siku arobaini … Matendo 1:3
Walipokuwa wakitazama, (Yesu) akainuliwa wingu likampokea kutoka machoni pao. Matendo 1:9
(Yesu) akachukuliwa juu mbinguni akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Mark 16:19
Yesu alipofufuliwa kwa uzima, Alimshinda njia ya kuepuke kutawaliwa na dhambi na hivyo kupokea msimamo wa sawa na Mungu.
Sasa hivi Yesu yu hai mbinguni pamoja na Baba yake, akifanya kupatikana kwa kuzaliwa upya na uzima wa milele kwa wote ukiwemo wewe, ambao watachagua kumpokea kama Bwana wa maisha yao.
Alipomfufua (Yesu) katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwenye wa roho Waefeso 1:20
Yesu) aweza kuwaokoa Kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye: maana yu hai siku zote ili awaombee (Kama wakili) Waebrania 7:25
SURA YA 4
Uzaliwe mara ya Pili sasa. Sasa ni siku ya wokovu wako! Usicheliwe!
Tazama, wakati uliokubaliwa ndio sasa; tazama siku ya wokovu ndiyo sasa 2 Wakorintho 6:2
Hauna budu kuzaliwa mara ya pili. Yohana 3:7
Kuzaliwa upya ni kipawa kutoka kwa Mungu kuja kwako. Kuzaliwa upya hakuwezi kufanyiwa kazi ili kupatikana; lazima kupokelewe kwa kuamini na kutendea Neno la Mungu, ukijua kwamba Mungu hawezi kudanganya. Atafanya kama neno lake litangazavyo.
Kwa neema, mmeokolewa kwa jina ya Imani (kuamini) ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha Mungu wala si kwa matendo ya mtu awaye yote asije akajisifu Waefeso 2:8,9
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele Yohana 3:16
Hakuna dhambi iwezayo kukutenga na Mungu isipokuwa kumkataa mwanawe, Yesu, kama mwokozi na Bwana.
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi” Warumi 5:8
Kuzaliwa mara ya pili ni tendo rahisi tu la moyo na kinywa.
Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Warumi 10:9
Ukiamini moyoni mwako ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na ya kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, kuzaliwa upya kwako kutatokea ghafla unapokiri Yesu kama mwokozi na Bwana wa maisha yako.
Roho mtakatifu ataunganika na Roho yako ya kibinadamu, akitia uzima halisi na asili ya Mungu mwenyewe kwa mtu wako wa ndani. Kwa wakati huo, Roho yako itafanywa mpya na takatifu, na kukupa msimamo wa sawa na Mungu na uzima wa milele.
Wengi wamedanganyika kwa kuamini kuwa wana uzima wa milele ati kwa sababu majina yao yamo kwenye orodha ya kanisani, wanafanya matendo mema au wamefuata desturi za kidini. Hata hivyo, mbali na kuzaliwa upya kulingana na maandiko, hakuna njia ya kuingia katika jamii ya Mungu na hivyo basi, hakuna uzima wa milele katika ufalme wa Mungu!
Basi, ikiwa hujuwahi kumpokea Kristo kama mwokozi na Bwana, au ukiwa una shaka kwamba umewahi kuzaliwa mara ya pili, lazima usuluhishe jambo hili kabisa, mbele ya mwumba wako.
Kwa wakati huu, chagua kuingia katika uhusiano na Mungu, na uanze kuishi katika utele sasa na hata milele!
Omba, ukikiri yafuatayo, ili ujisikie ukizungumza. Amini kila neno na moyo wako wate, na utazaliwa mara ya pili mara moja.
Mungu uliye mbinguni,
Naja kwako katika jina la Yesu. Naamini na moyo wangu kuwa Yesu Kristo ni mwana wako na kwamba ulimfufua kutoka kwa wafu.
Nakataa dhambi.
Nakataa ya kale.
Natubu na kugeuka kutoka kwa maovu.
Nachagua uzima!
Sasa ninampokea Yesu Kristo katika maisha yangu kama mwokozi wangu kutoka kwa dhambi, kutoka kuzimu na kutoka kwa nguvu za shetani.
Ninakukiri wewe Yesu kama Bwana wangu.
Kwanzia wakati huu na kuendelea, mimi ni wako.
Nitakufuata, Yesu, katika maisha yangu yote.
Wewe ni kiongozi na mwelekezi wangu!
Sitakuonea aibu, Bwana Yesu.
Nitakukiri mbele ya watu.
Naamini sasa hivi mimi ni mkriso!
Roho mtakatifu ameungnika na Roho yangu ya kibinadamu na sasa nimezaliwa mara ya pili.
Yesu ni mwokozi na Bwana wangu!
Asante Baba wa mbinguni, kwa kunipa uzima tele wa milele!
Katika jina la Yesu! Amina!
Sahihi----------------------------------
Tarehe --------------------------------- Saa ---------------------------
SURA YA 5:
Karibu kwa jamii ya Mungu.
Hongera (pongezi)! Tuna furahia kukukaribisha katika jamii ya Mungu. Kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi na Bwana wako ndio uamuzi wa muhimu ambao utawahi kufanya. Umechagua uzima. Sasa Mungu ni baba yako na wewe ni mwana wake milele. Yesu hatawahi kukuacha wala kukupungukia.
Roho yako sasa imeumbwa upya, imesafishwa na daima imekamilika. Una maisha mapya, yenye mwanzo mpya.
Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya
(II Wakorintho 5:17).
Nanyi amewahuisha (amewafanya kuwa hai na wapya), mliokuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu. (Waefeso 2:1)
-----Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
(II Wakorintho 6:16)
Kuzaliwa upya hakutegemezwi, katika hisia, bali ni kuwa umetenda neno la Mungu.
Sasa wewe ni ‘mpya’ katika Kristo Yesu, hutawahi kutengwa tena na upendo wa baba Mungu wako. Endapo shetani atakutia shaka kuhusu uhalali wa kuzaliwa kwako upya, kumbuka kuwa una neno la baba yako lisilobadilika kwa uzima wa milele.
Mungu hawezi kusema uongo--- (Waebrania 6:18).
(Kila mtu) amwaniniye (Yesu Kristo) atapata ondoleo (msamaha) la dhambi. (Matendo 10:43).
Amwaniye mwana (Yesu Kristo) yuna uzima wa milele---- (Yohana mtakatifu 3:36).
Kuonyesha kuzaliwa upya kwako, zingatia mtoto aliyezaliwa na mama ambaye hamtaki mtoto huyo. Sasa hebu wazia jamii iliyo bora sana; jamii inayopenda kutoa! Jamii hii inampenda mtoto aliyekataliwa, hatimaye inamchukua kama mtoto wao. Wanampa jina lao na kumtunza kama ni mtoto wao wa kumzaa.
Nini hasa kilitendeka katika tukio hili? Ni kama kwamba mtoto huyu alizaliwa upya, na kupokea wazazi wapya na urithi mpya! Kwa nini? Si kwa jambo lolote ambalo mtoto huyu alifanya lili kustahili nafasi kama hii, lakini ni kwa sababu wazazi walimpenda mtoto huyu wakampa kibali/upendeleo. Jukumu la mtoto si kuwalipa hao wazazi, lakini ni kuitikia kuzaliwa kwake upya kwa kupokea kwa shukrani yote ambayo jamii yake mpya inampa.
Ndivyo ilivyo na kuzaliwa upya kwako. Ukisha zaliwa mara ya pili, kusudia kupokea yote ambayo yamepeanwa kwako. Anza kutenda kama sehemu ya jamii ya Mungu, ukishiriki tunuku na majukumu ya urithi wako mpya.
----Mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani Baba (Warumi 8:15).
Roho (mwenyewe) hushuhudia pamoja na roho zetu (zilizozaliwa mara ya pili) ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi, warithi wa Mungu, Warithio pamoja na Kristo, (Warumi 8:16-17)
Tazama ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; (I Yohana 3:1)
SURA YA 6.
Peana umakini kwa neno la Mungu.
Kwa kuwa sasa umezaliwa mara ya pili, Roho yako ni mpya, ingawa mwili wako wa kawaida na nafsi yako havijabadilika. Hata hivyo, unavyozidi kuamini na kukiri neno la Mungu kila siku, nia yako itaendelea kuhuishwa upya, ikikuza ukubaliano kati ya nafsi na Roho yako iliyozaliwa mara ya pili.
Muungano huu wa nafsi na Roho kupitia neno la Mungu ni wenye nguvu. Utakutia nguvu ili utawale mwili wako, na hivyo basi, kutii mapenzi ya Baba yako wa mbinguni.
Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.
(Warumi 6:12).
Ninyi toeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai----wala msiifuatishe namna ya dunia hii, Bali mgeuzwe (Kwa njia gani?)--- kwa kufanywa upya nia zenu… Warumi 12:1,2.
Maana mlinunuliwa kwa thamani sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu (pia) katika roho zenu---- (I Wakorintho 6:20)
Neno la Mungu lililoandikwa, Bibilia, sasa, ndio kitabu chako cha uzima kwa kuwa kinatumika katika kila hali. Neno la Mungu likitendewa kazi katika upendo kila mara litakusababisha ushinde.
Kulitii neno la Mungu huchochea msaada wake wa kiungu kwa niaba yako, na Mungu akiwa upande wako, hakuna ambacho kitakushinda!
Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. (2 Timotheo 2:15)
Kila andiko lenye pumzi ya Mungu… ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. (2 Timotheo 3:16,17)
Neno la Mungu ni makala halali, yalifunikwa na damu ya Yesu. Baraka zilizo ndani yake ni za faida yako. Mungu anatamani kuwa wewe, mwana wake, upate furaha tele katika maisha haya, na hata katika miaka ijayo.
Unapopata andiko linaloelezea wewe ni nani na kile ulichonacho, katika Kristo, liamini na ulikiri na kinywa chako. Kataa, kuzungumza kinyume na kile ambacho neno la Mungu linatangaza kukuhusu! Ukiendelea kukubali ahadi na kweli hizi, basi zifanyika halisi katika maisha yako.
Yeyeto---aamini kwamba hayo asemayo yametukukia, yatakuwa yake.
Turuhusu tukusaidie katika huhuisha nia yako, na kukomaa katika Bwana, kwa kuuliza kukiri maandiko yafuatayo mara kwa mara.
Ninakiri na kinywa changu ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana wangu na naamini moyoni mwangu ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu; kwa hivyo nimeokoka. (Warumi 10:9)
Mimi ni mwana wa Mungu, nimezaliwa mara ya pili kwa mbegu isioyharibika ya neno la Mungu.
(IPetro 1:23)
Jina langu limeandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo. (Rev. 21:27)
Nimekombolewa kutoka katika nguvu za giza na kuhamishwa na kuingizwa katika ufalme wa mwana wa pendo lake. (I Wakolosai 1:13)
Mwili wangu ni hekalu la Roho mtakatifu: Sasa basi ninamtukuza Mungu katika mwili wangu na Roho yangu, vilivyo vya Mungu. (Wakorintho 6:19,20)
Mimi ninageuzwa kwa kufanywa upya nia zangu (Warumi 12:2)
Mungu hakunipa roho wa woga, bali ya nguvu na upendo na moyo wa kiasi (2 Timotheo 1:7)
Ninafanikiwa na ni katika afya, kama vile roho yangu ifanikiwavyo. (III Yohana2)
Ninamtwika Bwana fadhaa zangu zote, kwa maana yeye hujishughulisha kwa mambo yangu.
(I Petro 5:7)
Hatanipungikia kabisa wala kiniacha kabisa. (Waebrania 13:5)
Ninaenda kwa imani si kwa kuona. (II Wakorintho 5:7)
Ninayasahau yaliyo nyuma nikiyachuchumilia yaliyo mbele. (Wafilipi 3:13)
Tunda la roho yangu iliyozaliwa mara ya pili ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utuwema, fadhili, uanimifu, upole, na kiasi (Wagalatia 5:22,23)
Ninayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. (Wafilipi 4:13)
Ninampenda Mungu kwa maana alinipenda kwanza (I Yohana 4:19)
Mimi ni mtendaji wa neno wala si msikiaji tu. (Yakobo 1:22)
Yeye aliye ndani yangu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. (I Yohana 4:4)
Ninamtii Mungu, ninampinga shetani katika jina la Yesu na kwa neno la Mungu naye ananikimbia.
(Yakobo 4:7)
Ninamvaa Bwana Yesu Kristo wala siuangalii mwili hata kuwasha tamaa zake (Warumi 13:14)
Ninamtumaini Bwana kwa moyo wangu wote wala sizitegemei akili zangu mwenyewe. Katika njia zangu zote ninamkiri yeye naye ananyosha mapito yangu. (Methali 3:5,6)
Mimi ni hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. (Waefeso 6:10)
Mungu wangu atanijaza kila ninachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu. (Wafilipi 4:19)
Mimi ni mjumbe kwa ajili ya Yesu Kristo na kushiriki kwa ujasiri ukweli wa ufalme wake na wengine. (Wakorintho 5:20)
Nami ninashinda kwa damu ya mwanakondoo, na kwa neno la ushuhuda wangu. (Ufunuo 12:11)
Mungu akiwa upande wangu, nani aliye juu yangu? (Warumi 8:31)
Yeye aliyeanza kazi njema ndani mwangu ataimaliza. (Wafilipi 1:6)
Ninafurahi katika Bwana siku zote (Wafilipi 4:4)
Ninatafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote nitazidishiwa.
(Mathayo 6:33).
Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wangu ndipo nami nitafunuliwa pamoja naye katika utukufu. (Wakolosai 3:4)
Anza kutumia muda kila siku katika neno la Mungu, ukigundua haki zako, tunuku na majukumu yako kama Mkristo mpya. Jisimike kwa dhati katika ahadi za Mungu, ukijiona kama mshindi badala ya aliyeshindwa. Jinsi ambavyo chakula cha kawaida kinadumisha mwili wa kawaida, neno la Mungu hutia nguvu Roho na nafsi yako.
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyogoshiwa, ila kwa hayo mpate kuukulia wokovu. I Petro 2:2
Kwa kuzingatia neno la Mungu kwa bidii, Imani katika Mungu itakuwa na uwezo wa kupokea kutoka kwa Mungu utaongezeka.
Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Mungu. (Warumi 10:17)
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza (Mungu); kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.
(Waebrania 11:6)
SURA YA 7
Tembea katika nuru ya uzima. Ukisha zaliwa mara ya pili, lazima utembee katika nuru kila siku kwa kutii sehemu za neno la Mungu ambazo unazijua. Ukitenda kwa imani kila kweli ambayo imefunuliwa kwako, utaongezkeka, katika hekima na utadumu katika baraka!
Basi Yesu akwaambia wale….walioamwamini, “Ninyi mkikaa katika neno langu,---- mtaifahamu kweli, nayo hiyo kwele itawawela huru. (Yohana 8:31,32)
Yeye anifuataye (Yesu Kristo) hatakwenda gizani kamwe, Bali atakuwa na nuru ya uzima.
(Yohana 8:12)
Lakini iweni watendaji wa neno wala si wasikiaji tu----(Yakobo 1:22)
Mungu hatamani tu uhusiano na watoto wake, bali pia shirika. Hiki kilio cha moyo cha Baba wetu wa mbingunin kinatoshelezwa kupitia ushirika na watoto wake katika maombi.
Zaidi ya haya, kuliitia jina la Baba kupitia imani katika jina la Yesu humpa njia moja kwa moja ya kukutana na mahitaji yako. Ushirika na Baba ni muhimu katika kupata baraka za mbinguni ukingli duniani.
Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu (Yesu) (Yohana 16:23)
Katika kila neno kwa kusali na kuomba na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu
(Wafilipi 4:6)
Kama mwana mtiifu wa Mungu, waweza kuwa mshindi katika hali zote. Hata hivyo lazima usongelee ukomavu kwa kumfuata Yesu kwa dhati.
Kwa hivyo, ni muhimu kwamba ujiunge maramoja ujitlolee kuhudhuria kanisa la karibu ambapo Yesu anatukuzwa na neno la Mungu linatangazwa kwa mamlaka na nguvu.
Wala tusiache kukusanyika pamoja---- (Waebrania 10:25)
Pia, lazima ubatizwe katika maji kulingana na ahadi ya Yesu, kuonyesha kuachana na maisha yako ya kale na kukumbatia maisha mapya.
Basi, enendeni, mkwafanye, mataifa yote kuwa wanafunzi, mikwabatiza kwa jina la Baba, na mwana, na roho mtakatifu, (Matho yo 28:19).
Basi tulizikwa naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake: kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. (Warumi 6:4)
Kuishi katika nuru ni kutembea katika upendo wa Mungu. Ukisha zaliwa mara ya pili, asili yako ni upendo wa Baba yako wa mbinguni. Sasa una uwezo wa kuishi bila ubinafsi/uchoyo ukileta baraka kuu kwa wengine na ushindi kwako! Upendo utakufanya kile ambacho moyo wako umetamani. Ukifuata sheria ya upendo, huwezi kushindwa.
Kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminika katika mioyo yetu (Roho iliyozaliwa mara ya pili) na Roho mtakatifu tuliyepewa sisi. (Warumi 5:5)
Yeye ampemdaye…akaa katika nunu … (Yohana 2:10)
Upendo haupungui. …(I Wakorintho 13:8)
Bwana anajua kwamba, kama wakristo, hatuwezi kukoza kufanya makoa. Namna mtu hazaliwi akiwa amekomaa kimwili, vivyo hivyo ukomavu wa kiroho haudhihiriki ghafla.
Hasa katika miaka yako ya mwanzo ya kutembea na Bwana, waweza kupungikiwa katika viwango vilivyoonyeshwa katika neno la Mungu. Hata hivyo usishushwe moyo! Ungali mtoto wa Mungu, kwa upendo amepeana njia ya urejesho wa ushirika pamoja naye ambao kutotii huuzuia.
Iwapo utashindwa, omba msamaha mara moja kutoka kwa Baba yako wa mbinguni, ukijua kwamba yeye ni mwaninifu kulingana na neneo lake kukutakasa na kufuta kutoka katika kumbukumbu yake makosa yako yote. Jisamehe kila mara, na uendelee kufurahi, na ujue kuwa unakua katika neema na maarifa ya Bwana wetu Yesu Kristo!
Tukiziungama dhambi zetu, yeye (Mungu Baba) ni mwaninifu na wa haki hata atuondelee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (I Yohana 1:9)
SURA YA 8.
Pitisha nuru.
Kazi yako duniani leo ni kueneza uzima wa tele wa ajabu ambao Mungu amepeana. Chagua kuwa baraka!
Pitisha nuru ya neno la Mungu lililo katika kitabu hiki kwa wengine ambao huenda hawajazaliwa mara ya pili, au kwa wale ambao wana shaka kuhusu uhusiano wao na Baba wa mbinguni. Kama balozi wa Kristo, utaathiri maisha kukomboa watu kutoka katika giza hadi katika nuru ya milele!
Mmepata bure, toeni bure. (Mathayo 10:8)
Basi, kila mtu atakayenikiri (Yesu Kristo) mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni (Mathayo 10:32)
Ukisha chagua uzima wa Kristo – nenda na uishi!
Mungu uliye mbinguni,
Naja kwako katika jina la Yesu.
Naamini na moyo wangu kuwa Yesu Kristo ni mwana wako na kwamba ulimfufua kutoka kwa wafu.
Nakataa dhambi na ya kale.
Natubu na kugeuka kutoka kwa maovu.
Nachagua uzima!
Sasa ninipokea Yesu Kristo katika maisha yangu kama mwokozi wangu kutoka kwa dhambi, kutoka kuzimu, na kutoka kwa nguvu za shetani.

Sitakuaibikia, Bwana Yesu.
Nitakukiri mbele ya watu.
Naamini sasa hivi mimi ni mkristo!
Roho mtakatifu ameuganika na Roho yangu ya kibinadamu na sasa nimezaliwa mara ya pili.
Yesu ni mwokozi na Bwana wangu!
Asante, Baba wa mbinguni, kwa kunipa uzima tele wa milele!
Katika jina la Yesu! Amina!
Sahihi________________
Tarehe_______________ Saa______________
Nan Ragland anahudumu kama mhuduma wa Injili, akiwa aliitikia hadharini mwito wa Bwana katika huduma akiwa na umri wa miaka minane. Katika utiifu wa mwito huo, Nan amehusika kwa bidii katika namna mbalimbali za huduma ya hadhara tangu utotoni.
Hivi sasa Nan na mume wake husafiri kwa mwili wa Kristo wote akihudumu katika nyimbo na mahubiri ya kujenga, kuonya na kufariji. Madhihirisho ya Roho na nguvu huandamana na neno lililohubiriwa, likimtukuza Yesu na kukutana na mahitaji ya watu.
Kuongezea, Nan huhudumu katika kimataifa kupitia namna mbalimbali za kuwafikia watu, zikiwemo vitabu, majalida, na kanda za mafundisho. Shauku yake isiyozimika ni kutumika kama nuru iwakayo na kuangaza, ikiwatayarisha watu walioandaliwa kwa ajili ya Bwana!
Huduma ya Nan Ragland
S.L.P 77, Jackson, Ms 39205
(601) 355 – 7777